Kutokana na mlipuko wa gesi katika eneo la makazi huko Karachi Pakistan, watu 13 wamefariki na 14 kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Abna kwa chanzo kutoka gazeti la Dunya, watu 13 ikiwemo msichana mdogo walifariki kutokana na kuanguka kwa paa lililosababishwa na mlipuko wa chombo cha gesi katika eneo la Rana Colony Soldier Bazaar lililopo Karachi Pakistan.
Katika tukio hili pia watu 14 walijeruhiwa.
Vyanzo vya uokoaji vilitangaza kwamba mlipuko huu ulitokea kwenye ghorofa ya kwanza ya jengo na kusababisha kuanguka kwa sehemu ya jengo hilo.
Maafisa wa uokoaji walitangaza kwamba inashukiwa kuwa watu 2 wamenaswa chini ya vifusi.
Mashirika ya uokoaji na maafisa wapo katika eneo la tukio na uchunguzi zaidi unaendelea kubaini sababu halisi ya mlipuko huo.
Mashahidi wa macho walisema kwamba nguvu ya mlipuko ilikuwa kubwa kiasi kwamba majengo ya jirani pia yalitetemeka na hofu ilitanda katika eneo hilo.
Your Comment